Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Dec 13, 2016

Jumuiya ya Ulaya na Marekani zaiwekea vikwazo DRC kwa mauaji ya waandamanaji

Jumuiya ya Ulaya na Marekani zimeweka vikwazo dhidi ya maofisa wakubwa wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kuhusika na mauaji ya waandamanaji waliotaka Rais Joseph Kabila kuachia madaraka.

Jumuiya ya Ulaya imewataja maofisa saba wa usalama wakiwemo makamanda wa jeshi pamoja na wa polisi na kiongozi wa ulinzi wa Rais Kabila.
Marekani kwa upande wake wamewataja waziri wa mambo ya ndani wa DRC na mkuu wa intelijensia.
Serikali ya Kongo imetaja vikwazo hivyo kuwa sio halali.
Mamia ya watu waliuawa wakati wa maandamano yalioanza mwezi Septemba baada ya Rais Kabila kutangaza kusitishwa kwa uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwaka huu

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP