Jeshi la Syria limesema mapigano ya mjini Aleppo yapo katika hatua za mwisho baada ya kufanikiwa kudhibiti sehemu kubwa ya mji huo kutoka mikononi mwa waasi.
Mkuu wa kamati ya usalama Luteni Jenerali Zaid al-Saleh, amesema wapiganaji waasi hawakuwa na muda walitakiwa kusalimu amri au kufa.
Maelfu ya raia wanaaminika kuzungukwa na waasi, ambapo maji na chakula vimekwisha.

Vikosi vya serikali pia vilidhibiti eneo la Saliheen siku ya Jumatatu
Image captionVikosi vya serikali pia vilidhibiti eneo la Saliheen siku ya Jumatatu

Kwa sasa waasi wamepoteza zaidi ya asilimia 90 ya udhibiti waliokuwa nao mashariki mwa Aleppo tangu serikali ilipoanzisha operesheni mwezi uliopita kuhakikisha inaudhibiti kabisa mji huo kutoka kwa waasi.
Urusi, inayounga mkono serikali, imesema zaidi ya raia 100,000 wamekimbia makazi yao kutokana na mapigano na wapiganaji waasi 2,200 wamesalimu amri.