Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Dec 2, 2016

Kanye West aondoka hospitalini

Mwanamuziki Kanye West anaripotiwa kurejea nyumbani zaidi ya wiki moja baada ya kulazwa kutokana na uchovu.
Kulingana na taarifa tofauti nchini Marekani, mwanamuzi huyo aliondoka hospitali ya UCLA jimbo la Los Angels na mkewe Kim Kardashian pamoja na daktari wake Michael Farzam,

Kanye alilazwa hospitali ya UCLA jimbo la Los AngelsImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionKanye alilazwa hospitali ya UCLA jimbo la Los Angels

Kanye West mwenye umri wa miaka 39 alilazwa hospitalini siku ya Jumatatu bada ya kupatwa na uchovu uliotokana na kukosa usingizi na kuishiwa na maji mwilini, kwa mjibu wa TMZ.
Nalo jarida la People limenukuu taarifa zinazo sema kuwa Kanye yuko nyumbani akiwa anapumzika.

Kanye West alisitisha kwa ghafla tamasha lakeImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionKanye West alisitisha kwa ghafla tamasha lake

Alitumia karibu muda wa dakika kumi akizungumza kuhusu Beyonce, Jay Z, Hillary Clinton na mwanzilishi wa Facebook Mark Zuckerbrg wakati kifanya shoo.
Mwanamitindo Kendal Jenner, ambaye ni dada wa kambo wa Kim Kardashian, alisema kuwa familia imekuwa ikimuombea Kanye.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP