Tume ya umoja wa mataifa kuhusu haki za kibinadam imeonya kuwa mauaji ya kikabila yanaendelea nchini Sudan Kusini.
Tume hiyo iliyoundwa mwezi Machi mwaka huu na yenye wanachama watatu, imekamilisha ziara yake ya siku kumi nchini Sudan Kusini.
Mwenyekiti wa tume hiyo Yasmin Sooka amesema jamii ya kimataifa inastahili kuchuckua hatua za dharura kuzuia mauji ya kimbari kama ilivyotokea nchini Rwanda.

Watu wengi wameikimbia Sudan KusiniImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionWatu wengi wameikimbia Sudan Kusini

Taifa la Sudan Kusini limekumbwa na machafuko tangu mwaka wa 2013 baada ya kujinyakulia uhuru wake kutoka Sudan.
Ripoti hiyo iliyotolewa mjini Geneva, inasema kuwa mauaji ya kikabila yanaendelea katika maeneo kadhaa nchini humo.

Huenda mauaji ya kimbari yakatokea Sudan KusiniImage copyrightAFP
Image captionHuenda mauaji ya kimbari yakatokea Sudan Kusini

Ripoti hiyo imesema kuwa waathiriwa wanafariki baada ya kubakwa, kuteketezwa wakiwa hai katika vijiji vyao au hata kunyimwa chakula hadi kufa.
Tume hiyo imeonya kuwa ikiwa hatua ya dharuru haitachukuliwa basi huenda mauaji ya kimbari yakatokea nchini Sudan Kusini.