Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Dec 19, 2016

KONGAMANO LA VILABU VYA UMOJA WA MATAIFA UN LAFANA TANGA


 WANAFUNZI wa Vilabu vya Umoja wa Mataifa kutoka  vyuo Vikuu na Shule za Sekondari na Msingi kutoka Mikoa mbalimbali nchini wamekutana Tanga kujadili mambo mbali mbali yahusuyo shughuli za Umoja wa Mataifa.
Wanafunzi hao walijadili mambo hayo yakiwemo  Demokrasia na Utawala bora Barani Afrika pamoja na changamoto za Raia katika nchi zenye machafuko.
Pia walijadili uchafuzi wa mazingira kwa nchi zenye viwanda na uharibifu wa mazingira ya bahari kwa baadhi ya viwanda kumwaga sumu baharini.
Akizungumza katika kongamano hilo, Mlezi wa (YUNA) Mkoa wa Kilimanjaro, Fransiss Shelutete, amezitaka Serikali nchi za Afrika kuwachukulia hatua kali  uchafuzi wa mazingira .Mwenyekiti wa Vilabu vya Umoja wa Mataifa (YUNA) nchini Rahim Nassir, akizungumza kwenye kongamano la vilabu vya umoja wa Mataifa lililowashirikisha wanafunzi vyuo vikuu na kufanyika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga 


Wanachama wa vilabu vya Umoja wa Mataifa (YUNA) kutoka Mikoa mbalimbali nchini wakifuatilia kongamano lililohusisha wanafunzi wa vyuoni na Shule za Sekondari na Msingi na kufanyika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa  Tanga 
 Viongozi wa Vilabu  vya Umoja wa Mataifa UN kutoka Mikoa mbalimbali nchini wakiwa katika picha ya pamoja na wanachama kutoka maeneo mbalimbali nchini.


Mratibu wa klabu ya Umoja wa Mataifa (YUNA) Mkoa wa Kilimanjaro, Fransisis Shelutete, akizungumza kwenye kongamano la Vilabu vya Umoja wa Mataifa kutoka Mikoa mbalimbali nchini na kufanyika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Tanga

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP