Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Dec 15, 2016

MICHEZO YA TANO YA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI TANZANIA YATIMUA VUMBI TANGATanga, MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Deudence Kakoko, amewataka wafanyakazi wa mamlaka hiyo kufanya kazi kwa bidii ili kwenda kasi ya  Serikali ya awamu ya Tano.
Akifungua michezo ya Tano ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (INTERPORTS GAMES) viwanja vya shule ya Sekondari ya Popatlal Tanga jana, Kakoko, alisema kila mfanyakazi wa Mamlaka hiyo anapaswa kujua wajibu wake.
Alisema kasi hiyo iende sambamba na uboreshaji wa utoaji huduma bandarini na kuwa kivutio kwa wageni ili kuweza kuitumia kwa kushusha shehena zao bandari za Tanzania.
Michezo hiyo inashirikisha wafanyakazi wachezaji kutoka Tanga ambao ni wenyeji, Dar es Salaam,, Mtwara na Bandari za Ziwa.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP