| Mkuu wa majeshi ya ulinzi Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange amefanya ziara ya kikazi ya siku mbili kisiwani Mafia mkoa wa Pwani. Pamoja na mambo mengine Jenerali Mwamunyange ametembelea gati la Kilindoni Mafia na visiwa vidogo vya Shungimbili, Nyororo na Mbarakuni na kujionea shughuli zinazoendelea hapo. Pichani anaonekana Mbunge wa Mafia Mhe. Mbaraka Dau (fulana ya mistari) akitoa maelezo ya jinsi wananchi wanavyopata huduma katika gati la Kiindoni |
0 Comments