Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Dec 25, 2016

Ndege yaanguka na wanajeshi 92 nchini Urusi

Kuna hofu kuwa huenda abiria wote 92 wamefariki baada ya ndege ya jeshi la Urusi waliokuwa wakisafiria kuanguka baharini katika eneo la Black Sea.
Wizara ya Ulinzi ya Urusi, imesema kuwa imepata mabaki ya ndege hiyo baharibi kilomita moja unusu kutoka Sochi.
Ndege hiyo muundo wa Tupolev-154, ilikuwa na abiria 91, wakiwemo wanajeshi wa Urusi na kikosi cha bendi cha jeshi maarufu kwa jina Alexandrov Ensemble.
Walikuwa wanatazamiwa kupiga mziki wa bendi ya mkesha wa mwaka mpya katika kambi ya jeshi la wanahewa karibu na mpaka na Syria huko mjini Latakia.

kikosi cha bendi cha jeshi maarufu kwa jina Alexandrov Ensemble.Image copyrightAFP
Image captionkikosi cha bendi cha jeshi maarufu kwa jina Alexandrov Ensemble

Ndege hiyi ilipotea katika mitambo ya Rada, muda mfupi baada ya kupaa angani, kutoka kwenye uwanja wa hoteli moja iliyoko maeneo ya Black Sea huko Sochi.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP