Zaidi ya wasichana 20 wa shule ya Chibok, ambao walitekwa nyara na kisha kuachiliwa huru na wanamgambo wa Boko Haram, wameungana na jamii zao wakati huu wa siku kuu ya Krismasi.
Ni mara ya kwanza wao kurejeshwa nyumbani, tangu walipoachiliwa huru mwezi Oktoba mwaka huu.

Wasichana hao wamekuwa wakilindwa katika eneo la siri ili kuzungumza na watawala wa serikali ya Nigeria.
Zaidi ya wasichana 220 walitekwa nyara na Boko Haram mnamo Aprili ya mwaka 2014.
Zaidi ya wasichana 200 hawajulikani waliko huku mazungumzo yakiendelea ili waachiwe huru.