Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, ameitisha mazungumzo ya kitaifa yatakayomaliza vita vya vya miaka mitatu vya wenyewe kwa wenyewe.
Akihutubia bunge mjini Juba, amesema jopo la wataalam litaongoza mazungumzo hayo.

Hata hivyo, hakumtaja hasimu wake, ambae alikuwa makamu wa Rais, Riek Machar, ambae alikimbia baada ya mapigano kuzuka mnamo mwezi July.
Afisa wa umoja wa mataifa anaeshughulikia masuala ya haki za bindamu nchini Sudan Kusini ametahadharisha kuzuka upya kwa mapigano ambayo yatahatarisha usalama wa eneo zima.
Rais Kiir amekana taarifa za mara kwa mara zinazotuhumu vikosi vyake kuhusika na mauaji ya halaiki na ubakaji.