Kampuni ya Intaneti ya Yahoo inasema wavamizi wa mitandao waliiba data za zaidi ya ya watumiaji wake bilioni moja.
Tukio hilo linaaminika kufanyika mnano mwaka 2013.
Katika taarifa yake, Yahoo inasema uvamizi huo wa taarifa muhimu ni tofauti na ule ulioripotiwa mwezi Septemba mwaka huu, ambapo wavamizi hao waliiba taarifa kutoka kwenye akaunti mbalimbali za watumiaji zaidi ya milioni mia tano.

Taarifa za uvamivi wa Yahoo zilianza kutolewa mwaka 2013
Image captionTaarifa za uvamivi wa Yahoo zilianza kutolewa mwaka 2013

Imeongeza kuwa data zilizoibiwa zinajumuisha majina, anuani, namba za simu,tarehe za kuzaliwa pamoja na nywila (namba za siri).
Lakini kadi za malipo sambamba na akaunti za benki hazikuingiliwa.