Shule ya UJerumani nchini UturukiImage copyrightDPA
Image captionShule ya UJerumani nchini Uturuki

Ripoti za vyombo vya habari kwamba shule moja ya Ujerumani nchini Uturuki imepiga marufuku sherehe za Krismasi imezua hisia kali nchini Ujerumani licha ya mamlaka ya shule hiyo kukana hatua hiyo.
Kulingana na ripoti, wafanyikazi katika shule hiyo ya Lisesi iliopo mjini Istanbul waliambiwa kwamba tamaduni za Krisimasi na nyimbo za Carol hazitaruhusiwa tena.

Wajumbe walitaja uamuzi huo kama wa ''kushangaza na majuto makubwa''.
Lakini shule hiyo imesema kwamba ripoti hiyo sio ya ukweli .
Instabul Lisesi ni shule ya upili ambayo imekuwepo kwa zaidi ya karne moja na ina takriban walimu 35 wa Ujerumani wanaofadhiliwa na serikali ya Ujerumani.
Wiki iliopita ,uongozi wa shule hiyo uliwatumia barua pepe wafanyikazi wa shule hiyo ukisema hakuna kufunza sherehe na tamaduni za krismasi na pia hakuna nyimbo za krisimasi zinazofaa kuimbwa.
Picha za barua hiyo zilichapishwa na chombo cha Sueddeutsche Ziteung nchini Ujerumani.
Wanasiasa nchini Ujerumani walitoa hisia za kushangazwa na hasira.
Raia mmoja wa Ujerumani mwenye mizizi yake nchini Uturuki ambaye ni kiongozi mwenza wa chama cha Green Party ,alisema kwamba ''inaonekana kwamba rais wa Uturuki Reccep Tayyip Erdogan yuko tayari kuondosha uhuru wa kuabudu kwa kuwa anaamini kwamba uongozi wake unatishiwa na nyimbo za Krismasi''.