Mkurugenzi mkuu wa shirika la umoja wa mataifa kuhusu haki za kibinaadamu nchini Dr Congo ameambia chombo cha habari cha Reuters kwamba kuna ripoti 'zinazothibitishwa' kuwa watu 20 walifariki na waliuawa katika makabiliano na maafisa wa usalama mjini Kinshasa.
Kuhusiana na swala la vifo, 'hali ni mbaya sana' Jose Maria aliambia chombo cha habari cha Reuters.
Kulingana na mtandao wa Politico takriban watu watatu walikuwa wamedaiwa kuuawa na wanajeshi mjini Kinshasa.
Watu wengine watano walijeruhiwa, wawili vibaya baada ya kupigwa risasi wakiwa karibu na maafisa wa kikosi cha Republican Guard katika mji wa N'djili mojawapo ya wilaya zenye idadi kubwa ya watu.
Milio ya risasi bado inaendelea kusikika katika maeneo tofauti mji Kinshasa, licha ya kuwa kiongozi wa upinzani Etienne Tshisekedi ametaka kufanyika kwa maandamano ya amani, ripoti hiyo imeongezea.
Maandamano yamekuwa yakifanyika katika miji kadhaa ya DR Congo ambapo muhula wa rais Joseph Kabila uliisha siku ya Jumatatu.

Maandamano ya kumpinga kabila nchini DR Congo
Image captionMaandamano ya kumpinga kabila nchini DR Congo

Wakati huohuo kumekuwa na maandamano katika miji kadhaa mikuu duniani ya kumtaka rais wa DR Congo Joseph Kabila kujiuzulu.
Mapema siku ya Jumanne milio ya risasi iliendelea kusikika huku waandamanaji wakimtaka rais Kabila kujiuzulu.
Raia bado wanaendelea kupiga firimbi mjini Kinshasa.
Wanasema kuwa hatua hiyo inatoa ishara kwamba muhula wa Kabila umekamilika.
Pia wanaimba kwamba Kabila Must Go { kabila ni sharti aondoke mamlakani}, kulingana na ripoti za BBC