Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Jan 7, 2017

Ajali ya Basi la Mohammed Trans Yaua Watatu Manyoni, Singida

TAARIFA zilizotufikia hivi punde, zinaeleza kuwa basi la Kampuni ya Mohammed Trans limepata ajali mapema leo na kuua watu 3 huku wengine 6 wakijeruhiwa nje kidogo ya Mji wa Manyoni mkoani Singida.
Aidha, inasemekana kuwa basi hilo lilikuwa limekodiwa na walimu ambao walikuwa wakisafiri kutoka jijini Tanga.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, chanzo cha ajali hiyo ni gari dogo lililokuwa limeegeshwa barabarani bila tahadhari yoyote, mbele ya basi kulikuwa kuna lori la mafuta hivyo dereva wa lori alipoona mbele kuna gari limepaki na yeye akatanua kwa haraka.
Wakati huohuo, basi nalo lilikuwa linataka ku-overtake hivyo dereva wa basi akashindwa kulimudu kutokana na mwendokasi hivyo kuligonga lori la mafuta kwa nyuma na kutoboka kitu kilichosababisha kumwagika mafuta barabarani licha ya kwamba hayakushika moto.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP