Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Jan 7, 2017

Sajent Afunguka Tetesi Za Kutembea Na Darassa

sajent-3
MWAKA Mpya, Mpaka Home inaendelea kukupa burudani. Mungu ni mwema, katukutanisha tena hapa sehemu yetu pekee ya kujidai ambapo tunapata fursa kuyajua mambo mbalimbali ya mastaa wetu wayafanyayo nje ya kazi zao zilizowatambulisha kwa mashabiki wao.
darassa-11Darassa
Aliyetufungulia dimba mwaka huu ni mwanamama ambaye alishawahi kushiriki mashindano mbalimbali miaka ya 2000 kama Kimwana Manywele, Miss Singinda na hivi sasa ni muigizaji wa filamu za Kibongo, Husna Idd ‘Sajenti’ ambaye anaishi Sinza-Madukani jijini Dar.

sajent-4Nyumbani hapo alipopanga, anaishi na watoto wake wawili wa kike pamoja na ndugu zake wengine. Watoto hao kila mmoja ana baba yake. Mmoja amezaa na msanii wa filamu, Salim Ahmed ‘Gabo’, mwingine ni wa mwanamuziki, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’
sajent-5Ili kuweza kuyajua maisha yake kiundani zaidi mimi na wewe twende pamoja chini kwenye maswali na majibu.
sajent-6
Ilisemekana ameolewa vipi ndoa bado ipo?
“Mmmh mambo mengine ni magumu sana hata kuyaelezea lakini nashukuru Mungu, kwa sasa nafurahia maisha yangu japokuwa siishi na baba mtoto wangu ambaye watu wengi walikuwa wanajua kama nimefunga naye ndoa.
sajent-7
Anawezaje kulea watoto mwenyewe au mmoja wa baba mtoto wake anamsaidia?
“Hakuna hata mmoja anayejali kuangalia watoto hivyo mimi pamoja na dada yangu ananipa msaada mkubwa sana mpaka watoto wangu wanakua wala sihitaji tena kitu kutoka kwao maana maisha yangu yanaendelea kama kawaida.
sajent-8
Ni rafiki na jiko, vipi kuhusu kufua au kuosha vyombo?
“Sasa hakuna kitu nakipenda sana kama kupika na ninajisikia vizuri sana nikipata muda mzuri wa kupumzika nyumbani, napenda kupika mwenyewe na kuhusu kufua na kuosha vyombo hizo ni kazi za mwanamke lazima nizifanye hazikwepeki hata siku moja.
sajent-9
Anapokuwa nyumbani anapenda kufanya nini?
“Hapa nyumbani kuna watoto wengi ambao ni wadada yangu, kaka yangu hivyo furaha yangu nikiwaona napenda kucheza nao na muda mwingi unakuta niko nao tunakimbizana, tunaimba ili mradi tu watoto wafurahi.
sajent-10
Baba wa watoto wake walishawahi  kuja nyumbani kuwaona watoto wao?
“Hapana na hilo sihitaji sana kikubwa ninachotaka watoto wafahamu baba zao ni kina nani lakini mambo mengine wala  sihitaji tena acha iwe nilizaaga nao na wakanipa zawadi ya watoto wazuri wa kike.
sajent-11
Anazungumziaje tetesi za kutoka na Darassa kwa sasa?
“(Kicheko) Darassa ni mshikaji wangu kitambo sana sijamjua leo wala jana, nilijua tu ukaribu wetu lazima uzue jambo lakini hakuna kitu chochote.
sajent-12
Anapenda kupika nini, chakula gani anape-ndelea?
“Napendelea sana mchemsho wa kuku wa kienyeji pamoja na ugali na mboga  mbalimbali za majani na hata kukipika chakula hicho mimi ndiyo navutika nacho sana.
sajent-13
Mara ya mwisho kupanda daladala lini?
“Yaani kwa kweli sikumbuki hata kidogo na sababu kubwa siyo kwamba sipendi natamani sana kufanya hivyo ila unapopanda lazima huwezi kukaa kwa raha kila mtu atakuwa anakukodolea macho wewe tu.
sajent-14
Kitu gani anafanya nje ya sanaa cha kumuingizia kipato?
“Kuna biashara nafanya ya kuuza nguo za wadada mbalimbali ndiyo kitu mbadala baada ya kazi yangu ya sanaa, nashukuru sana inanisaidia watoto wangu wanaendelea na maisha yao ya kawaida.
sajent-1
Vipi kuhusu kupenda kuvaa nguo fupi?
“Kuvaa nguo fupi ni kitu ninachokipenda tangu zamani na hata watoto wangu wakiniona hivi inabidi wakubaliane na mimi na kama wao watavaa wala siwezi kuwakataza kabisa.

Nini matarajio yake ya mwaka huu?
“Kufanya kazi zaidi ili niweze kuwapa watoto wangu elimu bora na vitu vingi ambavyo wanastahili kupata kwani hata kama baba zao wamewatenga mimi nitapambana ili maisha yaende vizuri zaidi.”
Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP