Mbunge wa jimbo la mafinga
mjini Cosato Chumi akikabidhi mashuka kwenye moja ya Zahanati ilikuwa na upungufu wa mashuka katika kata ya Isalavanu
wakati wa ziara yake ya kukagua na kugundua changamoto za zahanati za jimbo la mafinga mjini





 Mbunge wa jimbo la mafinga
mjini Cosato Chumi kushoto akiwa na katibu wake pamoja na mfanyakazi wa zahanati matanana wakati wa ziara yake


 Mbunge wa jimbo la mafinga
mjini Cosato Chumi akiwasalimia wananchi wa kata ya Isalavanu
wakati wa ziara yake



Mbunge wa mafinga mjini akitandika moja 
ya shuka kati ya mashuka aliyoyagawa katika zahanati mbalimbali katika 
jimbo lake ,Mashuka hayo yametolewa na mfuko wa bima ya afya NHIF
Na fredy mgunda,Iringa



Mbunge wa jimbo la mafinga
mjini Cosato Chumi ametoa jumla ya mashuka mia moja (100) kwenye zahanati,vituo
vya afya na hospitali ya mafinga kwa lengo la kuboresha huduma za kiafya kwa
wananchi wanaopata huduma katika maeneo hayo.


Akizungumza na blog hii mbunge
huyo alisema kuwa aliomba mashuka kutoka mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF)kwa
lengo la kuboresha huduma za kiafya katika jimbo la mafinga mjini.


“Zahanati na vituo vya afya
vingi vinachangamoto nyingi lakini moja wapo ni kukosekana kwa mashuka ya kutosha
kwenye maeneo mbalimbali ya kiafya hivyo nilichukua jukumu la kwenda mfuko wa
taifa wa bima ya afya (NHIF)kuomba 
msaada wa mashuka na namshukuru mungu wamenisaidia na kunipa mashuka
haya yote”. Alisema Chumi


Aidha Chumi aliwataka
watendaji wa sekta ya afya katika jimbo la mafinga kuwahudumia wagonjwa kwa
weledi wao ili kuifanya kada hiyo kuondokana na changamoto ambazo zimekuwa
zikiwakumba mara kwa mara kutoka kwa wananchi.


“Nimeleta mashuka haya
naomba mtumie na kuyatunza ili yaweze kudumu kwa muda mrefu kwa kuwa ni mashuka
yenye ubora wa hali ya juu kama mnavyoyaona lakini boresheni huduma kwa kutoa
huduma nzuri kwa wananchi hapo ndio wananchi watafurahia serikali yao”.Alisema
Chumi


Chumi aliwashukuru mfuko wa
taifa wa bima ya afya (NHIF)kwa kuwapa mashuka hayo ambayo yamefanikiwa kutatua
changamoto ya ukosefu wa mashuka katika jimbo la mafinga na amewaomba wazidi
kuwasaidia wananchi wa jimbo hilo.


Kwa upande wao viongozi wa
zahanati hizo walimshukuru mbunge wa jimbo hilo Cosato Chumi kwa kujituma na
kutafuta njia za kutatua changamoto kwenye zahati zote za jimbo la Mafinga
mjini tofauti na ilivyokuwa hapo awali kwa viongozi wengine.


“Unaona toka ameingia
madarakani amekuwa akiwaleta viongozi mbalimbali wa serikali ili kutafuta njia
za kutatua changamoto za huduma za afya,alimleta naibu waziri wa wizara ya afya
na maendeleo ya jamii Hamis Kigwangala na wengine wengi kwenye sekta nyingine”.
Walisema viongozi hao


Baadhi ya madiwani
waliendelea kujivunia juhudi za mbunge wao kwa kazi kubwa anayoifanya kuwaletea
maendeleo katika jimbo la Mafinga Mjini ambapo hapo awali ilikuwa vigumu
kushudia  mbunge akijituma kama
anavyofanya Cosato Chumi


Naye mwenyekiti
wa halmashauri ya Mji wa Mafinga Charle Makoga amesema kuwa changamoto ya huduma
ya afya katika vijiji vya jimbo la Mafinga ni mbaya na inahitaji juhudi binafsi
kuwasaidia wananchi na kuongeza kuwa tatizo la umeme ni kubwa katika vijiji
ambavyo havipokupata umeme wa REA awamu ya kwanza na pili na ndio sababu
inayosababisha huduma za kiafya kudorola katika baadhi ya vijiji.