Maandamano makubwa kutoka kwa makundi ya wanawake dhidi ya Donald Trump yamekuwa yakifanyika Australia,New Zealand na Japan.
Maandamano makubwa zaidi yamefanyika mjini Sydney, Australia,ambako karibu watu elfu tatu wameandamana kuelekea katika ubalozi wa Marekani nchini humo. Waandamanaji

wanampinga Bw. Trump hasa juu ya madai ya mwenendo wake wa kuwakosea heshima wanawake.
Nchini Marekani pia kumeshudiwa katika mji wa Washington wakati wa hafla ya kuapishwa kwa Donald Trump kuwa Rais wa 45 wa taifa hilo.
Polisi mjini huo walilazimika kutumia gesi ya kutoza machozi kwawatawanya waandamanaji huku baadhi yao wakiharibu magari na na hata kuyachoma moto.
Maadamano mengine mia saba sawia na hayo yanapangwa kufanyika leo katika miji mingine mikuu Duniani.