Madaktari sita kutoka muungano wa madaktari nchini Kenya wamepewa muda wa wiki mbili kumaliza mgomo wao la sivyo wafungwe jela wiki mbili.
Mgomo huo ambao umeendelea kwa zaidi ya mwezi mmoja umeathiri pakubwa shughuli za matibabu katika hospitali za umma.
Mahakama ya Ajira na mahusiano ya kazi nchini Kenya imeamuru muungano wa madaktari kusitisha mgomo huo na kumaliza mazungumzo na serikali katika kipindi cha wiki mbili zijazo.

Madaktari wa Kenya wakiwa katika mkutano
Image captionMadaktari wa Kenya wanaogoma wakiwa katika mkutano wa kuangalia nini cha kufanya baada ya mahakama kuwaamuru wasitishe mgomo

Juhudi kadhaa za kumaliza mgomo huo zimegonga mwamba huku madaktari wakitaka kutekelezwa kikamilifu kwa mkataba uliosainiwa baina yao na serikali mwaka 2013 ili kuboreshwa kwa malipo na hali bora za kazi.
Jaji Hellen Wasilwa amesema kuwa iwapo maafisa watakaidi amri ya mahakama watafungwa jela wiki mbili.