Maelfu ya watu nchini Iran wamejitokeza kwenye mji mkuu Tehran kwa mazishi ya rais wa zamani Akbar Hashemi Rafsanjani.
Kiongozi wa Iran Ayatollah Ali Khamenei aliongoza maombi kwenye sherehe hizo.
Rafsanjani ambaye alikuwa rais kati ya mwaka 1989 na 1997 aliaga dunia kutoka na mshutuko wa moyo siku ya Jumapili akiwa na umri wa maika 82.
Alikuwa mmoja wa watu wenye ushawishi mkubwa tangu yafanyike mapinduzi ya mwaka 1979.
Raia wakiwa na picha za Akbar Hashemi Rafsanjani mjini TehranHaki miliki ya pichaEPA
Image captionRaia wakiwa na picha za Akbar Hashemi Rafsanjani mjini Tehran
Televisheni ilionyesha umati mkubwa wa waombolezaji katika mitaa inayozunguka chuo kikuu cha Tehran ambapo maombi yanafanyika.
People attend the funeral ceremony of Akbar Hashemi Rafsanjani in Tehran, Iran (10 January 2017)Haki miliki ya pichaREUTERS
Rafsanjani alikuwa muungaji mkono wa rais wa sasa wa Iran Hassan RouhaniHaki miliki ya pichaAFP
Image captionRafsanjani alikuwa muungaji mkono wa rais wa sasa wa Iran Hassan Rouhani
Raia wa Iran wakikusanyika kando ya gari lililokuwa limebeba jeneza la Rafsanjani mjini Tehran.Haki miliki ya pichaAFP
Image captionRaia wa Iran wakikusanyika kando ya gari lililokuwa limebeba jeneza la Rafsanjani mjini Tehran.