Watu kadha wanahofiwa kuaga dunia baada ya mashua iliyokuwa safarini kutoka mji wa bandari wa Tanga ikielekea kisiwa cha Pemba kuzama Jumatatu usiku.
Kamanda polisi eneo la kaskazini mashariki, Benedict Wakulyamba, aliiambia BBC kuwa mashua hiyo ilikuwa imewabeba watu 50.

Mkuu huyo wa Polisi alisema kuwa watu tisa wameokolewa na miili 12 kupatikana.
Kilichosababisha kutokea ajali hiyo hakijathibitishwa lakini kamanda wa polisi anasema upepo mkalia huenda ulisababisha mashua hiyo kupoteza mwelekeo.