Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Jan 13, 2017

Marekani kuanza kudai viza raia wa Cuba

Marekani imesitisha sera ya muda mrefu ambayo ilikuwa inawapa raia wa Cuba hadhi maalumu ya kuingia na kuishi nchini Marekani bila ya visa.
Serikali ya Cuba imekuwa ikilalamika kwamba, sera hiyo, ijulikanayo kama "wet foot, dry foot," imewafanya maelfu ya raia wa Cuba kukimbia nchini humo kila mwaka.

Rais Obama amesema hatua ya kuondolewa kwa sera hiyo, ni hatua muhimu katika kurudisha uhusiano na Cuba.
Mahasimu hao wa muda mrefu wamerudisha uhusiano wa kidiplomasia mnamo mwaka 2015 baada ya karne ya uhasama.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP