Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Jan 2, 2017

Mlipuaji awaua watu 4 Somalia

Habari kutoka mji mkuu wa Somalia, zasema kuwa watu wanne wameuwawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa baada ya mlipuaji wa kujitoa kufa alipojilipua karibu na uwanja wa ndege mjini Mogadishu.

Idara ya Polisi imesema kuwa, mhanga huyo aliyevalia vilipuzi na kuweka mabomu ndani ya gari alilokuwa akiliendesha, alilipua bomu hilo katika kizuizi chya barabarani mita chache karibu na uwanja wa ndege wa Somalia mjini Mogadishu.
Kapteni Mohamed Hussein amesema kuwa walinda usalama walikuwa wakilipekuwa gari hilo ndipo likalipuka mita 100 kutoka makao makuu ya majeshi ya muungano wa Afrika ya kulinda amani AMISOM. Pia eneo hilo ni karibu na Hoteli ya amani.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP