Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Jan 2, 2017

Wanadiplomasia wa Urusi waliotimuliwa Marekani waondoka

Vyombo vya habari vya Urusi vimeripoti kuwa wanadiplomasia 35 wa Urusi waliotimuliwa na rais Barack Obama kutoka Marekani wameondoka wakiandamana na familia zao.
Urusi ilituma ndege maalum ya kuwarudisha nyumbani.
Wanadiplomasia hao waliamuriwa kuondoka Marekani baada ya Urusi kushtumiwa kuwa ilijaribu kuingilia uchaguzi wa hivi majuzi wa Marekani kwa njia ya udukuzi wa mitandaoni.
Vyombo vya kijasusi vya Marekani vinadai kuwa utawala wa Urusi ndio ulioamuru kudukuliwa kwa hasa tovuti ya chama cha Democratic ili kuvuruga kapeni za bi Clinton na kumsaidia Donald Trump ambae sasa ndiye rais mteule.CHANZO: BBC SWAHILI

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP