Na
Woinde Shizza,Arusha.


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema kuwa serikali
haitasita

kuwachukulia hatua wawekezaji wanaochochea migogoro katika wilaya ya

Ngorongoro na kusababisha uvunjifu wa amani hivyo kuchangia kuzorota kwa

shughuli za maendeleo.






Gambo ameyasema hayo katika ziara yake wilayani Ngorongoro inayolenga

kutatua migogoro wa pori tengefu lenye ukumbwa wa kilomita za mraba elfu

kumi na tano ambapo amekutana na wadau mbalimbali ikiwemo

wawekezaji,wafugaji pamoja na viongozi wa kiserikali.





Amesema kuwa serikali itawaondoa wawekezaji wanaochochea migogoro na

kuwagombanisha wananchi na serikali yao jambo ambalo halitafumbiwa

macho





Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Rashid Taka amesema kuwa wako baadhi ya watu

wanaonufaika na migogoro hiyo hivyo kumalizika kwa migogoro hiyo kutaleta

manufaa kwa wananchi wengi kuliko kunufaisha kundi la watu

wachache





Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo,Kilimo na Uvuvi
ambaye

pia ni Mbunge wa Ngorongoro Wiliam Ole Nasha na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa

Arusha  Lekule Laizer wamesema kuwa utatuzi wa mgogoro huo utasaidia

kuepusha migongano ya kimaslahi na kuchochea shughuli za kimaendeleo
badala

ya kutumia muda mwingi katika usuluhishi wa miigogoro hiyo






Mkuu wa Mkoa ameanza Ziara yake leo Wilayani Ngorongo na kesho atatembelea

katika vijiji mbalimbali ikiwa ni katika juhudi za kutatua mgogoro wa pori

tengefu katika wilaya hiyo.