Na Woinde Shizza,Arusha

Wakuu wa
mashirika umeme kutoka katika nchi kumi za Afrika zinazozalisha

umeme(Eastern Africa Power pool(EAPP)     
  zimekutana  jijini arusha

kwa malengo ya kujadili mfumo wa usafirishaji wa umeme ikiwa ni pamoja na

namna wananchi wao watakavyoweza pata nishati ya umeme kwa uraisi tofauti

na sasa




Hayo yalisemwa na naibu katibu mkuu wizara ya nishati na madini
Dkt.Juliana

palangyo alipokuwa akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa wakuu wa

mashirika ya umeme katika nchi hizo za eastern Africa power

pool(eapp)mapema leo



Palangyo alisema kuwa lengo halisi ni kuweza kujadili mambo mbalimbali

yahusuyo nishati ya umeme kwa watumiaji wake kwani  kuna
uwezekano  mkubwa

wa nchi zote zilizo kwenye umoja huo.



Alisema kwa sasa yapo baadhi ya makampuni ambayo yalikuwa yanauza
umeme kwa

gharama kubwa hasa kwa wananchi ambao hawajapata huduma hiyo ya umeme

lakini kupitia umoja huo wataweza kupata nishati hiyo kwa gharama
nafuu.



"Hizi nchi za eastern tumekutana hapa ili tujadili namna ambayo tunaayo

wanayoweza kutafuta namna ya kuzalisha umeme kwa bei nafuu na kisha nchi

hiyo itaweza kuuza umeme  kwa bei ndogo"aliongeza
palangyo.



Hataivyo kwa upande  kaimu meneja uhusiano wa shirika la
tanesco  Leila

Muhaji alisema kuwa katika mkutano huo pia watajadili namna ambavyo

tanzania itajenga njia ya usafirishaji wa umeme wa njia ya maji ambayo

itatoka nchi ya tanzania kwends kenya,zambia,pamoja na nchi
nyingine



Muhaji alisema kuwa tanzania itanufaika na ujenzi wa njia hizo hivyo
jamiii

itanufaika kwa kiwango kikubwa sana kama ilivyo kwenye nchi ambazo

zimeeendelea duniani.



"Hataivyo mara baada ya huu mkutano wa wakuu wa nchi zinazolisha umeme

tunatarajia pia kuwepo na wadau wengine ambao ni mawaziri kutoka nchi zote

ambao nao sasa wataweza kuweka mambo sawa ili huduma iweze kumfikia

mlengwa"aliongeza Muhaji

Alimalizia kwa
kutaja nchi ambazo zina unda umoja huo kuwa ni  Tanzania
,Kenya,Uganda ,Rwanda ,Burundi ,Sudan , Dr congo, Ethiopia ,Djbout,
Libya pamoja na Egypt.