Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, amepuuzilia mbali madai ya Korea Kaskazini kuwa imeunda Kombora linaloweza kuwasilisha zana za nuklia hadi Marekani.
Katika mawasiliano kupitia mtandao wa Twitter, Bwana Trump aligusia majigambo ya kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, katika ujumbe wake wa mwaka mpya ambapo alisema kuwa maandalizi ya kombora la aina hiyo yamefikia hatua ya mwisho.

Bwana Trump alisema katika ujumbe wake kuwa "Haitawezekana." Tamko lake la haiwezekani, halikueleweka vizuri kwa sababu wachanganuzi hawajui iwapo alimaanisha kuwa Korea Kaskazini haina uwezo huo au alikuwa akiandaa hatua ya kujikinga.