Urusi inasema kuwa madai kuwa Marekani iliendesha kampeni ya udukuzi wa mitandao ili kushawishi uchaguzi wa urais nchini Marekani si kweli.
Msemaji wa serikali ya Urusi Dmitry Peskov aliwaambia waandishi wa habari kuwa Urusi imechoshwa na madai hayo.
Alisema kuwa ripoti iliyotolewa na mashirika ya ujasusi nchini Marekani kuhudu madai hayo haina msingi wowote.
Hayo ndiyo matamshi ya kwanza kutoka Urusi tangu rais mteule Donald Trump akabidhiwe ripoti hiyo.
Trump amekuwa akipinga madai ya udukuzi wa Urusi tangu ashinde uchaguzi wa urais mwezi Novemba.
Lakini mkuu wake wa jeshi Reince Priebus, amesema kuwa Trump amekubali matokeo ya uchaguzi ambayo yaliwasilishwa kwake na wakuu wa ujasusi.
"Hajakana kuwa urusi ilihusika kwenye masuala fulani," Priebus alisema.
Hata hivyo hakufafanua ikiwa Trump aliamini ripoti kuwa rais wa Urusi Vladimir Putin alikuwa ameamrisha udukuzi huo kufanyika.
Bwana Trump alitaja mkutano wa Ijumaa na wakuu wa ujasusi kuwa wenye manufaa, na kusema kuwa ataomba kati kipindi cha ndani ya siku tisini ofisini, kufanyika mpango wa kuzuia udukuzi wa mitandao.
Donald Trump alikutana na maafisa wakuu wa ujasusi akiwemo jenerali James Clapper (kulia)Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionDonald Trump alikutana na maafisa wakuu wa ujasusi akiwemo jenerali James Clapper (kulia)