mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro,wakati akiofungua Maonyesho
ya zana za kilimo  katika viwanja  vya Taasisi ya Utafiti wa kilimo ya Seliani 

 Afisa mauzo wa kampuni ya Irrico Saimoni Manyike   akimuelewesha mkulima jinsi kampuni yao inavyofanya kazi ya kusambaza teknolojia ya umwagiliaji wa Matonye
 Washiriki ambao ni wakulima wakifuatilia kwa makini mada ambazo zilikuwa zikiendelea wakati wa ufunguzi

   Habari picha na Woinde Shizza,Arusha




sekta
ya kilimo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo  ufugaji holela , ambao  hupelekea uharibifu wa mazingira,Teknolojia duni
pamoja na ugumu wa kupata mitaji ya kuboresha miundombinu ya kilimo.







Hayo
yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro,wakati akiofungua Maonyesho
ya zana za kilimo  katika viwanja  vya Taasisi ya Utafiti wa kilimo ya Seliani  vilivyopo ndani ya jijini Arusha ambapo ni
mara ya kwanza kufanyika  .







Alisema
kuwa sekta ya kilimo inakabiliwa na changamoto za ufugaji holela ambao
unasababishwa na wafugaji ,wakulima kutumia teknolojia duni au zazamani katika
ukulima  pamoja na wakulima wengi kukosa
mitaji ya kubesha miundo mbinu ya kilimo







Alisema
kuwa hii inachangia kwa kiasi kikubwa kukwamisha maendeleo ya sekta hii
kutokana na wananchi wengi kutumia kilimo cha kawaida badala yakutumia kilimo
cha kisasa ambacho kinaleta tija .







“hapa
Tanzania zaidi ya asilimia 75% wanategemea kilimo lakini kati yao n asilimia
1.5 tu ndio wanatumia kilimo  cha kisasa
kama kilimo cha umwagiliaji ,kupanda mbegu
bora  pamoja na kilimo cha matone
hivyo ni vizuri wakulima wetu kujitaidi kutumia kilimo cha kisasa ili kuweza
kufanya kilimo chenye tija ambacho kinamnufaisha yeye mkulima mwenyewe na
kuachana na kilimo cha kawaida au naweza sema cha kienyeji”alisema Daqarro







Alisema
kuwa watanzania tunauwezo wa kuzalisha
mazao bora kwakuwa tuna aridhi nzuri ,maji mengi ya kutosha tunayo kwani
tunamito mingi inayotoa maji  hivyo
tukiamua kuwekeza na kulima kilimo chakisasa tunaweza kusaidika na hata   pato la mkulima litakuwa na sio mkulima tu
na pia pato la serikali pia litaongezeka kutokana na kilimo.



















Aidha
mkuu huyo wilaya alisea kuwa serikali inawashukuru wadau kwa kuupa mkoa wa
Arusha heshima ya kufanyika kwa maonyesho hayo ambayo yatafanyika kwa muda wa
siku mbili hivyo amewataka wananchi wajitokeze kwa wingi katika kujifunza
teknolojia mpya za kilimo na ubunifu wautaalamu mbalimbali .















“napenda
pia kuwataka  waonyeshaji kuangalia suala
la bei kwani  asilimia 75-80 ya wakulima
ni wakulima wadogowadogo hivyo ni vyema wakauza bidhaa zao kwa bei nafuu ili
wakulima wa hali ya chini aweze kumudu kununua bidhaa ili waweze kuendana na
kasi ya kilimo cha kisasa ,Serikali kwa kushirikiana na wadau wa kilimo
wanaangalia ni kwa namna gani



wataweza
kuboresha sekta hii ya kilimo kwa kutoa elimu mbalimbali kwa wakulima ili
kuepukana na kilimo duni ambacho kinasababisha hasara kwa wakulima nchini”alisema
Daqorro



















Kwa upande wake mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti ya Seliani
Dr Daniel Mafuru   amesema kuwa wamekua
wakishirikiana na wadau mbalimbali wa kilimo ,katika uzalishaji wa Teknolojia
,pamoja na kuwatafutia wadau wa kilimo masoko ya mazao yao.







Aidha alisema kuwa
Seliani wapo  tayari kuwaunganisha
wakulima na waonyeshaji wa teknologi ,ilikuwawezesha wakulima kupata mafunzo na
kubadilishana ujuzi  pia iwapo watauwaunganisha
itawasaidia  kufahamu namna ya kuhifadhi
mazao yao baada ya uvunaji ili wasipoteze mazao kama ilivyokuwa kabla ya kupata
elimu hiyo ya kilimo.







 Kwa meneja masoko wa
kampuni ya John Deere ambaye pia ndio wadhamini wakuu wa maonyesho haya Wayne Travas
alisema kuwa kampuni yao  zinatefaya kazi
ya kuwaletea wakulima wadogo mashine za kilimo ambazo zitawasaidia kufanya kazi
vizuri  na kwa teknologia za kisasa
pamoja na ubora
mwingi.




 mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti ya Seliani
Dr Daniel Mafuru
  Akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa maonyesho hayo
 Washiriki wakifuatilia


 meneja masoko wa
kampuni ya John Deere ambaye pia ndio wadhamini wakuu wa maonyesho haya Wayne Travas Akifafanua jambo  mbele ya waandishi wa habari
 katika maonyesho haya pia kamera yetu  iliweza kumkuta mwimbaji mashuhuri wa jijini hapa Nakaya Sumari akiwa na Phidesia Mwakitalima nao pia waliuthuria  katika maonyesho hayo ili nao waweze kulima kilimo chenye tija
 Baaadhi ya wakulima wakiangalia matrekta ya kisasa yanayouzwa na kampuni ya John Deere nambao ni wathamini wakuu


 Mmoja wa mkulima akiangalia jinsi ngowe zilizolimwa kwa njia ya matone zilivyostawi shambani
 Afisa mauzo wa kampuni ya Irrico Saimoni Manyike akiwaonyesha wakulima hawapo pichani jinsi  kilimo cha umwagiliaji wa mtone kinavyokuwa




Mshauri wa sekta ya kilimo na ufugaji  David Nyange akifafanua jambo katika uzinduzi wa maonyesho hayo