Nchini Serbia, safari zote za mashua katika mto Danube zimesitishwa.
Viwango vya joto katika baadhi ya maeneo ya Urusi vimeshuka hadi nyuzi joto -40C (-40F).
Ugiriki, ambayo kawaida huwa haishuhudii majira mabaya zaidi ya baridi, viwango vya joto maeneo ya kaskazini vimefikia -15C (5F). Katika maeneo hayo, mhamiaji kutoka Afghanistan alifariki kutokana na baridi wiki iliyopita. Barabara katika eneo hilo zimefungwa.
Mjini Athens, kiwango cha joto kilikosa kupita 0C mwishoni mwa wiki, na visiwa vingi eneo hilo vimefunikwa na theluji.
Baadhi ya visiwa vya Ugirini vimekuwa makao ya maelfu ya wahamiaji ambao sasa wanahamishiwa makao mapya ya muda au mahema yenye mitambo ya kuongeza joto.
Haki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGESImage captionMji wa Istanbul, Uturuki ulipigwa na dhoruba kali ya barafu mwihoni mwa wikiHaki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGESImage captionBaadhi ya maeneo ya kusini mwa Italia yamefunikwa na theluji, unaweza ukafikiria ni SiberiaHaki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGESImage captionSanamu na chemchemi za maji Roma vimefunikwa na thelujiHaki miliki ya pichaEPAImage captionKambi ya wahamiaji katika kisiwa cha Lesbos nchini UgirikiHaki miliki ya pichaAPImage captionWatoto wamepata fursa nadra ya kucheza juu ya maji ya mto Esca yaliyoganda na kuwa barafu eneo la Burgui, kaskazini mwa Uhispania
Majumba zinaowahudumia watu wasio na makao nchini Italia sasa yanafunguliwa usiku na mchana kuwahudumia watu wasio na makao.
Watu watano kati ya saba waliofariki nchini humo walikuwa watu wasiokuwa na makao.
Viwanja vya ndege Sicily, Bari na Brindisi vilifungwa mwishoni mwa wiki.
Hali pia si nzuri mjini Roma.
Na nchini Urusi, Moscow kulikuwa na baridi kali zaidi katika kipindi cha miaka 120 siku ya Krismasi ya kanisa la Orthodox tarehe 7 Januari.
Safari za ndege zilifutwa au kuahirishwa mjini Moscow.
Shule katika baadhi ya maeneo zilifungwa Jumatatu, ingawa maafisa wanasema hali itaimarika siku chache zijazo.
Haki miliki ya pichaEPAImage captionWaliofika eneo la Red Square, Moscow walihitajika kujifunika vyema na kuvalia mavazi yenye kuhifadhi joto kutokana na baridi kaliHaki miliki ya pichaEPAImage captionLicha ya baridi kali, mashindano ya kila mwaka ya baiskeli majira ya baridi yalifanyika MoscowHaki miliki ya pichaREUTERSImage captionNchini Ukraine, watu waliokuwa wakitembea kwa miguu pamoja na madereva walitatizika kuona kutokana na theluji Kiev
Mji wa Prague katika Jamhuri ya Czech ulipata usiku wa baridi kali zaidi usiku wa kuamkia leo. Watu watatu walifariki, wawili kati yao wakiwa watu wasiokuwa na makao.
Nchini Poland, watu 10 walifariki Jumapili na sasa maafisa wanasema idadi ya waliofariki kutokana na baridi tangu tarehe 1 Novemba wamefikia 65.
Miji ya Warsaw na Krakow ilitangaza Jumatatu kwamba wachukuzi wangeruhusiwa kusafiri bila kulipa nauli.
Haki miliki ya pichaAPImage captionMchonga barafu mjini Warsaw nchini Poland ambapo viwango vya joto vimefikia -14C
0 Comments