Binti wa Rais wa Marekani Ivanka Trump, amesema kuwa anaungana utawala wa baba yake kama mfanyakazi katika ofisi ya umma, kufuatia fununu kuwa ana nafasi nyeti ndani ya ikulu ya nchi hiyo.

Katika taarifa yake siku ya Jumatano, amesema kuwa anajua kuhusiana na fununu hizo, licha ya kusema kuwa alikua akijitolea tu kwa maadili yote.
Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa Ivanka Trump amepewa nafasi nyeti ndani ya ikulu ya Marekani akihusiana na masuala ya ulinzi wa ndani licha ya yeye kukanusha mara kwa mara.