Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana amesema migogoro ya ardhi katika Mkoa wa Dodoma itapatiwa ufumbuzi hivi karibuni kutokana na kushirikisha wataalamu wa sheria kuipitia na kutoa mapendekezo.
Alisema hayo juzi wakati akizungumza kwenye kikao kazi cha makamanda na maofisa waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini.

Alisema Mkoa wa Dodoma umeunda Kamati ya wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kushughulikia migogoro hiyo.
“Migogoro mingi imekuwa ikiangaliwa kisiasa, lakini tuliona umuhimu kama ikitafsiriwa kisheria, tuliomba wataalamu wa sheria kutoka Udom, watusaidie katika hili hata tukiingia kwenye maeneo hayo kutakuwa na ufumbuzi wa kudumu,” alieleza Rugimbana.
Alisema wanaamini tafsiri za kisheria kwenye migogoro ya ardhi itakuwa dawa ya kumaliza changamoto hizo ambayo iko kwenye maeneo mengi.
Alisema Dodoma ina vijana wengi wa vyuo vikuu ambapo wengi ni waathirika wa dawa hizo. Alitaka Rais John Magufuli asaidiwe na kuungwa mkono katika vita dhidi ya dawa za kulevya.