Kundi la Al-Shabab limewaonya wazazi nchini Somalia kutowapeleka watoto wao katika shule na vyuo vikuu visivyokuwa vya Kiislam.
Limedai kwamba elimu ya mfumo wa kimagharibi inazorotesha maadili

Msemaji wa kundi hilo Ali Mohamoud Rage katika ukanda wa video uliyorekodiwa dakika ishirini na sita, amesema mtu yeyote atakayejihusisha na elimu inayoeneza mila na tamaduni za kigeni atakabiliwa vilivyo.
Wanadai elimu ya kimagharibi haihimizi tabia ya maadili mema na kwamba ndio inayowapa motisha raia wa Kisomali kuhamia ulaya.
Hivi karibuni al-Shabab lilizindua mtaala wake wa elimu kwa lugha ya kiarabu.
Kwa upande wake serikali ya Somali imelishtumu kundi hilo kwa kujaribu kuwanyima watoto wa Kisomali elimu bora huku wakitaka kuwaingiza kwenye itikadi yao inayoendeleza mapigano na mauaji.