Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Apr 21, 2017

Ibrahimovic na Rojo wapata majeraha

Mkufunzi wa klabu ya Manchester United Zlatan Ibrahimovic na beki Marcos Rojo walipata majeraha ya miguu katika ushindi wa mechi ya ligi ya Yuropa dhidi ya Anderlecht.
Ibrahimovic mwenye umri wa miaka 35, alianguka vibaya alipokuwa akipigania mpira, huku RoJo mwenye umri wa miaka 27 akitolewa kunako dakika ya 23 baada ya kugongana na mchezaji mwengine.

Mkufunzi Jose Mourinho alisema kuwa habari za mapema kuhusu majareha hayo hazikuwa na ukweli.
Aliongezea: Nataka kusubiri lakini hisia zangu sio nzuri kwa wote wawili. Nataka kusubiri na kuwa na matumaini lakini siwezi.
Ibrahimovic ambaye alifunga mabao 28 msimu huu tangu uhamisho wake kutoka Paris St -germain, bado hajakubali kuongeza muda wake katika klabu hiyo.
Jereha la Rojo linamaanisha anajiunga na mabaki wengine Chris Smalling na Phil Jones katika orodha ya wachezaji wa United wenye majeraha.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP