Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akiwasisitiza walimu juu
ya utunzwaji wa madarasa ya shule ya Msingi Msakuzi katika dhifa ya
makabidhiano ya madarasa





Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisaini kitabu cha
wageni Mara baada ya kuwasili shule ya Msingi Msakuzi katika dhifa ya
makabidhiano ya madarasa
 Madarasa matatu ya shule ya Msingi Msakuzi yaliyokabidhiwa kwa MD Kayombo
Baadhi ya watumishi wa Manispaa ya Ubungo walioshiriki kwenye dhifa ya makabidhiano ya madarasa ya shule ya Msingi Msakuzi


Na Nasri Bakari, Dar es salaam



Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo amekabidhiwa
madarasa matatu yaliyokamilika na mkandarasi katika shule ya msingi
Msakuzi.



Makabidhiano ya madarasa
hayo ambapo ujenzi wake umegharimu shillingi millioni sitini na mbili
(62 Mil) yamefanyika katika shule hiyo iliyopo katika Kata ya Mbezi
Manispaa ya Ubungo.



Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo
Mkurugenzi Kayombo amesema kuwa amefurahi kuona ujenzi wa madarasa hayo
umemalizika kwa wakati na kutoa ahadi mbalimbali katika shule hiyo.



"Kwanza napenda nichukue fursa hii kukupongeza mkandarasi kwa kumaliza
ujenzi ndani ya muda tuliokubaliana kwa hakika umeonyesha ni jinsi gani
unajali kazi yako" Alisema MD Kayombo.



MD Kayombo amesema kuwa
mpaka kufikia kesho tarehe 06/04/2017 madawati 120 yanapaswa kufikishwa
kwenye shule hiyo huku akisema kuwa kila darasa yanapaswa kukaa madawati
arobaini(40) kila chumba katika vyumba vitatu vya madarasa
alivyokabidhiwa.



Pia ameahidi kuweka tarazo katika vyumba viwili
vya madarasa ya zamani ambapo pia ameahidi kutoa mifuko Hamsini ya
Saruji kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa ofisi ya walimu na kuahidi
kuhakikisha shule hiyo inakuwa ya mfano.



"Fedha hizi za kununua
mifuko ya Saruji nitatoa kwenye mshahara wangu hivyo namsihi Mheahimiwa
Diwani wa eneo hili naye aweze kuchangia ujenzi huu" Alisema MD Kayombo
 "Tunakushukuru
sana Mkurugenzi kwa jitihada ulizozionesha katika shule hii kwa kipindi
kifupi kwa kutununulia eneo la shillingi Millioni 35 na kutujengea
madarasa matatu mungu akubariki sana" Alisema Bi Shahiri.



Mkurugenzi Kayombo amewasihi walimu wa shule hiyo kujitahidi kutunza
mali za serikali zikiwemo madarasa, madawati na samani nyingine.