Mkurugenzi
mwenza wa Tanzanite One,Faisal Juma pamoja na viongozi wa serikali na
wajumbe  wa kamati ya shule ya Songambele  akikagua madarasa ambayo
hayatumiki  kutokana na nyufa baada ya shule kukumbwa na mafuriko na
kutangaza kujenga madarasa  saba.







Mkurugenzi mwenza wa Tanzanite One,Faisal Juma akizungumza katika
mkutano na wazazi wa shule ya msingi Songambele  ambayo ina uhaba wa
madarasa na kutangaza kujenga madarasa  saba Mwaka huu ili kupunguza tabu waipatayo wanafunzi hao kwa kukoisa vyumba vya madarasa.


ANDREA NGOBOLE; PMT
Siku tatu baada ya
kuripotiwa shule ya msingi Songambele iliyopo Mererani wilaya ya
Simanjiro, yenye wanafunzi 1126 kusoma katika madarasa manne,Kampuni ya
Tanzanite One imetangaza kujenga madarasa saba ili kuondoa uhaba wa
madarasa katika shule hiyo.

Mkurugenzi
mwenza wa kampuni ya Tanzanite One,Faisal Shabhai amesema,baada ya
kuona kwenye vyombo vya habari shida ya madarasa katika shule
hiyo,wameamua kujitokeza kujenga shule hiyo.

Shabhai
alisema,Tanzanite one kama mwekezaji Katika migodi ya Tanzanite
wanawajibu wa kusaidia masuala ya kijamii hasa kwa kuwa wananufaika na
madini ya Tanzanite.

"Tunajua tunawajibu wa kusaidia jamii hivyo tutajenga madarasa  saba katika shule hii"alisema

Katibu Tawala wa wilaya ya Simanjiro,Zuwena Omar  alishukuru kampuni Tanzanite One kwa msaada waliotoa kujenga madarasa hayo.

Omar alitoa wito kwa wawekezaji wengine waliopo Mererani kusaidia maendeleo ya Mererani.

Mwalimu
Mkuu shule hiyo.Mwanahamisi Mussa alisema wanakabiliwa na tatizo la
uhaba wa madarasa, matundu 40 ya vyoo,Nyumba za walimu na ofisi kwani
wanafanyakazi chini ya miti.