Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisaini kitabu cha
wageni Mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Ofisi Mtendaji wa Kata ya
Ubungo, kushoto ni Ofisa Mtendaji wa Kata Ya Ubungo Ndg Isihaka Waziri



Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akitoa maelekezo kwa Ofisa Mtendaji wa Kata ya Ubungo kuhusu namna ya kuyatoa marobota yaliyobaki baada ya kuwagawia wananchi vyandarua

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akiongea na baadhi ya watumishi aliowakuta ofisini

Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akikagua eneo La Ofisi ya
Mtendaji wa Kata ya Ubungo Mara baada ya kuwasili katika Ofisi hiyo




Na Mathias Canal, Dar es salaam



Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo Leo April 6,
2017 amefanya ziara katika Ofisi ya Ofisa Mtendaji Kata ya Ubungo ili
kujionea utendaji kazi katika Ofisi hiyo.



Akizungumza na baadhi
ya watumishi Mara baada ya kukagua eneo la Ofisi hiyo MD Kayombo Alisema
kuwa amefanya ziara hiyo ya kushtukiza ili kujionea hali ya ufanisi wa
kazi na kubaini kama kuna watumishi ambao hawafanyi kazi ya kuwatumikia
wananchi kwa weledi na badala yake wanafika ofisini Asubuhi kwa ajili ya kusaini na hatimaye wanaondoka.



"Watumishi wengi hutumia muda mwingi kufanya kazi zao badala ya kufanya
kazi za utumishi wa wananchi, Japo nawapongeza katika Ofisi hii
mmeendelea kuwa waumini wazuri wa kazi na ufanisi wenu unawasaidia
wananchi kuzidi kuiamini serikali yao" Alisema MD Kayombo



Akiwa
Ofisini hapo MD Kayombo ameagiza Marobota ya vyandarua zilizobaki ambazo
zilitolewa kwa ajili ya kuwagawia wananchi kutotolewa hovyo ama
kuhamishwa badala yake zitolewe kwa utaratibu mahususi utakaoelekezwa na
Ofisi ya Mkurugenzi.



Robota hizo zipo 34 katika Ofisi hiyo ya
Mtendaji wa Kata ya Ubungo zimesalia nyingi kutokana na wananchi wengi
kutojitokeza kuzichukua kutokana na sababu mbalimbali.



MD Kayombo
pia ameelezea mpango kabambe wa Manispaa ya Ubungo juu ya Ofisi hiyo ya
Mtendaji kubomolewa na hatimaye kuwa na uwekezaji mkubwa ambao
utaongeza wigo wa ukusanyaji mapato ya Manispaa hiyo.