Ngoma Africa band na muziki wao imetua kwa Wayaudi kutumbuiza sherehe za uhuru Yom Haatzmaut

Habari nyeti zimevuja kuwa Ngoma Africa band aka FFU bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya yenye mako kule ujerumani
inatua nchini Israel kutumbuiza katika onyesho maalum la siku ya uhuru wa nchi ijulikanayo kama  Yom Haatzmaut siku ya tarehe 1 mpaka 2 Mai 2017 mjini Tel Aviv,mmoja ya wanaitifaki wa maonyesho hayo Bi.Shimone amesema bendi hiyo ndio ya kwanza ya kiafrika kupata mwaliko wa kutumbuiza katika maonyesho hayo lakini akutaka kuelezea zaidi.Habari za uhakika zimevuja kuwa bendi hiyo imesafiri kimya kimya kutoka ujerumani kuelekea kwa wayaudi kwa ajili ya onyesho.