Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Apr 14, 2017

Washukiwa 4 wa mauaji ya polisi Tanzania wauawa

Maafisa wa polisi wa Tanzania wamewaua watu wanne wanaoshukiwa kuhusika katika mauaji ya maafisa wanane wa polisi katika usiki wa Alhamisi kusini mwa mji wa Dar es Salaam.

Kamishna wa polisi anayehusika na uchunguzi Nsato Mssanzya amesema katika mazungumzo na vyombo vya habari kwamba wanne hao walipigwa risasi muda mfupi Ijumaa alfajiri wakati wa msako.
Maafisa waliouawa waliripotiwa kushambuliwa walipokuwa wakipiga doria katika mji huo
Kamishna huyo alisema kuwa bunduki nne zimepatikana kutoka kwa washukiwa waliouawa ikiwemo bunduki mbili zilizoibwa kutoka kwa polisi waliouawa, huku operesheni ya kuwasaka washukiwa waliosalia ikiendelea.
Inspekta jenerali wa polisi Ernest Mangu alianzisha uchunguzi siku ya Alhamisi usiku.
Tayari rais Magufuli ameshutumu mauaji hayo na kutaka uchunguzi kufanywa.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP