Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

May 21, 2017

ALLY QWIDO NA STAM WAFANYA DUA MAALUMU YA KUWAOMBEA WAZAZI WAO WALIOTANGULIA MBELE YA HAKI LEO JIJINI ANTWERPEN UBELGIJI

Shekh Hassan ambaye ni mmoja wa mashekh wetu wakubwa nchini Ubelgiji akifungua rasmi dua ya kuwarehemu wazee wa wenzetu waliotangulia mbele ya haki.Shughuli hii imefanyika jijini Antwerpen.

Ally Qwido wa katikati mwenye kofia ya rangi ya udongo na tasbih mkononi akishiriki kumuombea dua marehemu mzee wake aliyetangulia mbele ya haki siku za hivi karibuni.Dua hii makhususi iliandaliwa kwa ajili ya Ally Qwido na Stam

Al-Ustadh Habib nae ni mmoja wa mashekh wetu wakubwa tunaowategemea nchini Ubelgiji,akitoa mawaidha na kutukumbusha umuhimu wa kujua maana ya umauti.

Waungwana toka sehemu mbalimbali walishiriki kwenye duaa za kuwarehemu wazee wa wenzetu

Na kwa upande wa kina dada na mama zetu nao walishiriki vyema katika dua ya leo.

Na kwa upande wa kina dada na mama zetu nao walishiriki vyema katika dua ya leo.

Wakati mawaidha ya kutukumbusha umuhimu wa kujua umauti kina mama na dada zetu walikuwa tulii wakisikiliza kwa umakini zaidi

Na kwa upande wa kina baba nao kama kawaida utulivu ulishika nafasi yake.

Mawaidha yakiendelea

Ustadhi Stam mmoja wa wahusika wakuu wa shughuli hii ya kuwaombea wazee waliotangulia mbele za haki..Stam nae alimpoteza mzee wake siku chache zilizopita.Kwa niaba ya familia zao whusika waliwashukuru kila mmoja aliyeshiriki kwenye kisomo.
{Picha zote na maelezo toka Maganga One}

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP