wakwanza  kushoto ni muaandaji wa
bonanza la Afya kwanza akiwa na timu ya Triple a klabu Fc  kabla
ya mechi kuanza(habari picha na Woinde Shizza wa
libeneke la kaskazini )









timu ya tigo Fc ikiwa pamoja na timu
ya Triple A klabu FC 


 waimbaji wa bendi ya Ricker
nest music band wakiwa katika picha ya pamoja na rais wa bendi hiyo
alkievaa nyeupe
 wachezaji wa timu ya Triple a
wakiburudika mara baada ya mechi kuisha
 waimbaji wa timu ya Ricker nest
music band wakiwa na mmoja wa washabiki wao wa music wao wakifurahi
pamoja
 timu ya mringa ringa
iikiendelea kufanya mazoezi kabla ya kuingia
uwanjani
 timu ya wavuta kamba ikiendelea
kuvuta kamba








 warembo wakifuatilia mpira kwa
makini
 timu ya Triple A wakiwa
wanapeana mawazo katika kipindi cha mapunziko
 wadau mbalimbali waliouthuria
bonanza hilo wakiendelea kupata vinywaji
 mmoja ya wachezaji wa timu ya
Triple A klabu Fc akiwa anatolewa uwanjani na wauguzi mara baada
yakuumia wakati akicheza
 Timu ya Tigo Fc ikiwa katika picha ya
pamoja kabla ya mechi baina yao na timu ya Triple A Klabu Fc kuanza





Na Woinde
Shizza,Arusha









Timu ya
Triple A klabu imelazimika kutoka sara ya bao moja
kwa moja na timu ya Tigo FC  katika
bonanza la michezo lijulikanalo kwa jina la Afya Kwanza
 lililofanyika katika viwanja vya Gymkana
jijini  hapa




 Bonanza
hilo ambalo
ni mara ya kwanza kufanyika limeandaliwa na
mkurugenzi wa Bendi ya Rickernest music band ,bendi ambayo makao makuu
yake ni jijini hapa na imeshirikisha michezo mbalimbali ikiwemo kuvuta
kamba  pamoja na mpira wa miguu









Akiongelea
bonaza hilo muandaaji wa mashindano hayo
Denis  Mtedeki   alisema
kuwa nia rasmi ya kuandaa bonanza hili ni kuwakutanisha watu
mbalimbali  na kufurahi pamoja  pamoja na kushiriki michezo
  ,ikiwa kama ni sehemu ya kufanya
mazoezi









Alisema kuwa
 bonanza
hili limeshirikisha jumla ya timu za mipira wa miguu mbili pamoja na timu
zingine mbili ambazo zilifanya kazi ya kuvuta kamba,alizitaja timu hizo kuwa ni
timu kutoka kampuni ya simu ya Tigo
(Tigo Fc), Olemringaringa FC, Red Apple,Mijada Fc  pamoja na
Triple a klabu FC.




 Denis
aliongeza kuwa
mbali na kushiriki bonanza hili pia wachezaji na washiriki waliouthuria
walipata fursa ya kupima magonjwa mbalimbali ikiwemo kupima presha na kisukari
bure.









Aidha
aliongeza kuwa bonanza hili alitaishia hapa bali
litakuwa likifanyika kila mwisho wa mwezi lengo ikiwa ni kufanya mazoezi
,kuwakutanisha wadau mbambali mbali na kufurahi pamoja