Mkuu wa mkoa wa Manyara
Dk Joel Bendera akifatilia
jambo wakati alipokuwa anazindua rasmi maonyesho ya sita ya vito na
madini yanayofanyika katika hotel ya Mounti Meru ilipo jijini
Arusha(habari picha na Woinde
Shizza,Arusha)





 Meya wa jiji la Arusha naye
aliuzuria katika uzinduzi wa maonyesho haya ya vito na madini






Na Woinde
shizza,Arusha









 wananchi wengi wanaoishi karibu na
migodi
mbalimbali inayochimba madini  ya aina
mbalimbali wamekuwa hawanufaiki kupitia madini hayo kutokana na viongozi wao wa
maeneo husika kutokuwa na  usiano mzuri
na wamiliki wa migodi hiyo.









Hayo yamebainishwa na mbunge wa jimbo la
Simanjiro Jemsi ole
milya wakati akiongea katika uzinduzi wa maonyesho   vito na
madini  yaliofunguliwa leo jijini
hapa









Alisema kuwa japo kuwa madini mengi yenye
dhamani yanachibwa
hapa nchini lakini ukifuatilia maisha ya wananchi wa maeneo ambayo
madini hayo hayafanani
kabisa nao kwani asilimia kubwa ya wananchi hao ni maskini sana
na wengine awajiwezi









“asilimia kubwa  ya
wananchi ambao madini hayo yanachibwa ukifatilia maisha yao hayafai kwani ni
duni  hawana maendeleo  yoyote ,kwa ufupi awanufaiki na madini ambayo
yanatoka katika maeneo yao hivyo ni wajibu waserikali kuangalia upya swala hili
na kuanza kufatilia kwani ni kitu cha kusikitisha unakuta mwananchi mfano wa
mererani madini yanachibwa kwao lakini ukiangalia maisha anaoyoishi uwezi sema
anakaa sehemu Tanzanite inatokea kwa jinsi anashida”alisema
Milya









Naye  kaimu naibu
katibu mkuu wa wizara ya Nishati na madini Jemsi Mdoe  alisema
kuwa sera ipo na sheria ipo ya
kuakikisha wananchi ambaowanazunguka maeneo ya migodi
wanasaidiwa  na migodi hiyo lakini ukifuatilia kwa kiasi
kikubwa wale wananchi ambao hawanufaiki ni wale ambao unakuta viongozi wao wa
mtaa au kijiji awanaushirikiano mzuri na viongozi au wawekezaji waliowekeza
katika maeneo yao ,hivyo ni wajibu wawanchi pamoja na viongozi kurikiana kwa
pamoja na kuungana ili kuweza kusaidia









Akizungumzia maonyesho haya ya vito na
madini   (Arusha Gem Fair )alisema kuwa haya ni
maonyesho ya sita kufanyika na yanafanyika kwa muda wa siku
tatu   lengo ikiwa 
kutimiza dira iliopo  katika sera
ya madini ya mwaka 2009  inayosisitiza
kuwa Tanzania iwe kitovu cha madini .









Alisema kuwa sekta ndogo ya vito inachangia
katika uchumi wa
maendeleo ya jamii  hivyo maonyesho
haya  ni fursa kwa wachimbaji  na wafanyabiashara wa hapa
nchini kuweza
kupata fursa ya kujitangaza zaidi









“unajua  wageni wengi
kutoka nchi mbalimbali wanauthuria katika maonyesho haya wengine wanakuja
kununua madini wengine wameleta madini yao ili yauzwe kwaiyo hii ni fursa ya
pekee ya wachimbaji wetu wa ndani kujitangaza na kupanua soko la zaidi kikubwa
zaidi  waangalie ni namna gani
watayafanya madini yao yawe na dhamani zaidi”alisema
Jemsi




 baadhi ya madini yaliyoletwa
katika maonyesho