Ligi kuu ya soka ya England imeendelea tena ,jana jumatatu kwa mchezo mmoja ,ambapo Vinara wa Ligi Chelesa wamepepetana na Middlesbrough na kuibuka kidedea kwa goli tatu bila upinzani.

Chelsea inayo nafasi moja tu kufikia kileleni mwa ligi baada ya kuichabanga timu ya Middlesbrough kwa bao tatu kiduarisho katika uwanja wa Stamford Bridge.
Antonio Conte aliwabugiza Middlesbrough kwa magoli baada ya kupokea pasi iliyotakata kutoka kwa Diego Costa, Marcos Alonso na Nemanja Matic, na huenda Chelsea watatawazwa kuwa vijogoo wa ligi kuu ya England endapo watafanikiwa kuvuka kihunzi katika uwanja wa West Bromwhichalbion siku ya ijumaa.
Chelsea walicheza kwa kujiamini mithili ya mabingwa, hata kama hawatashinda mwishoni mwa wiki dhidi West Brom , Chelesea inakabiliwa na mechi za nyumbani watford na Sunderland kujishindia taji la pili katika misimu mitatu.
Chelsea walishajitengenezea mazingira ya ushindi kabla hata Diego Costa hajageuza mchezo na yeye kuwa nyota wa mchezo baada ya kugongewa pasi murua na Cesc Fabregas katika dakika ya ishirini na tatu ya mchezo.
Mchezo ulinoga zaidi wakati Marcos Alonso alipopachika bao lingine kwa kuunyakua mpira miguuni mwa kipa wa timu ya Middlesbrough Brad Guzan dakika kumi na moja kabla ya kipyenga cha mapumziko .
Naye Cesc Fabregas iliingizia Chelesea goli la tatu na la lala salama.