Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

May 8, 2017

Emmanuel Macron rais wa Ufaransa

Emmanuel Macron ameshinda Uchaguzi wa Urais wa Ufaransa. Matokeo yanaonesha Macron amemuacha mbali mpinzani wake Bi Marine Le Pen kwa kujinyakulia asilimia 65 ya kura. Maelfu ya wanaomuunga mkono Macron walisherehekea katika kati mwa Paris wakipeperusha Bendera. Akiwa na miaka 39, Macron anakuwa Rais mdogo zaidi wa kuchaguliwa kuwahi kuiongoza ufaransa na wa kwanza kuchaguliwa kutoka nje ya vyama viwili vikubwa.

Katika taarifa yake, amesema kwamba Ufaransa imefanikiwa kufungua ukurasa mpya katika historia yake na kwamba alikuwa na ndoto ya kuwa mpiga mbiu wa nchi hiyo kwa kugunduliwa upya kwa matumaini na imani.Mshndi huyo wa nafasi ya urais ametoa hotuba yale ya kwanza akiwa ni raisi mteule. Emmanuel Macron, amenukuliwa akisema kwamba atahakikiksha anafanya kila linalowezekana kulipa fadhila ya uaminifu wa wafaransa waliompa.
Wafaransa wenzangu, mlioko ndani na nje ya ufaransa, baada ya vita ya muda mrefu vya kidemokrasia , na kuchagua kuweka imani yenu juu yangu. Ningependa kuchukua fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa heshima kubwa.
Macron anasema ni heshima kubwa na mmenipa wajibu mkubwa wa kutekeleza, bila kauli yoyote kwangu, natoa shukrani zangu za dhati kutoka ndani ya moyo wangu.shukrani hizi zimfikie kila mmoja wenu, kwa kura yako na kuniunga mkono. Sitasahau kwamwe, nitakuwa muangalifu sana na nitahakikisha kwa nguvu zangu zote naheshimu imani yenu kwangu.
Lepen amempongeza Macron kwa njia ya simu. Na kusema kwamba chama chake cha National Front kimepata ushindi mkubwa kwa kugawana kura, na kufanikiwa kuigawa Ufaransa kati ya wazalendo na watawala.
Marine Le Pen aliyekuwa na matumaini ya kuikwaa nafasi ya rais wa Ufaransa tayari amekubali kushindwa dhidi ya mpinzani wake Emmanuel Macron .watu wa Ufaransa wamemchagua rais wa Jamhuri, na wameamua kuwa na muendelezo . Nimempigia simu bwana Macron kumpongeza kutokana na ushindi wake
kwasababu nina wiwa moyoni mwangu na nina itakia mema nchi hii.Nimemtakia mafanikio mema katika changamoto zinazoikabili Ufaransa.Ningependa kuwashukuru raia wa Ufaransa milioni kumi na mmoja , ambao waliamua kunipa mimi sauti zao na imani yao juu yangu, pamoja na wanaharakati, ambao waliniunga mkono na kunipa ushirikiano wakati wote wa kampeni,nina furaha kubwa, kwasababu ni ushindi mkubwa kwa ulaya yote, ni ushindi kwa ulaya, ni mkubwa.
wafaransa walionesha furaha yao; ni ushindi mkubwa wa asilimia sitini na tano , hatukulitarajia hilo, naaa, ndo hivyo, ni utawala mwingine kwa Ufaransa. Huwezi kuamini, nina matumaini kwamba naamini atapata uungwaji mkono katika bunge la uchaguzi mnamo mwezi june na huenda ukaleta mabadiliko makubwa nchini. itastaajabisha.
Marina naye alisikika akisema; nimeridhika sana, ushindi huu umeiokoa Ulaya, nastaajabia kabisa, ni suala halisi, naamini itasababisha ulaya ijichekeche, nafikiri italeta mabadiliko makubwa , tutashuhudia mabadiliko makubwa yakiambatana na maelekezo mapya, ni ajabu, mastaajabu, asante.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP