NHIF
TANGA KUPELEKA HUDUMA YA TOTO AFYA KADI VIJIJINI


MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya
mkoani Tanga (NHIF) unakusudia kuwafikia wananchi kwenye vijiji na kata
mbalimbali mkoani hapa ili kutoa elimu juu ya umuhimu wa huduma ya afya
kwa watoto (Toto Afya  Kadi) ambapo uelewa wake umekuwa sio mzuri.




Hayo yalisemwa na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga
(NHIF) Ally Mwakababu (Pichani Juu)wakati akizungumza na mtandao huu
ofisini kwake ambapo alisema wameamua kufanya hivyo ili kuipa uelewa
jamii kuhusiana na umuhimu na faida za huduma hiyo.


Alisema wakiwa huko watapita kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo mashuleni
na kufanya mikutano ya nje kwa wananchi ili kuweza kuwapa uelewa juu
manufaa ya kuwaingiza watoto hao kwenye mfuko huo.



“Unajua hii huduma Toto Afya Kadi hasa kwa maeneo ya vijijini uelewa
wake umekuwa sio mzuri hivyo sisi tumepanga kuanza kuhamasisha na kuipa
uelewa jamii ili waweze kuitambua na kujiunga nayo “Alisema.



“Nia kubwa ni kutaka kuona jamii waliochini ya miaka 18 wana jiunga na
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwani itawasaidia kupunguza gharama za
matibabu kwa sababu akishajiunga anaweza kupata matibabu bure “Alisema.



Sambamba na hilo alisema pia hivi sasa wanaihamasisha jamii kuendelea
kujiunga nao ikiwemo wajasiriamali na vikundi vilivyosajiliwa ili kuweza
kunufaika na huduma zinazotolewa na mfuko huo.



“Lakini pia tunaendelea kuhamasisha wakina mama kujiunga na mradi wa KFW
mradi ambao unaendelea kwenye mikoa ya Mbeya na Tanga  kwani
itawasaidia kupata matibabu pindi wanapokuwa wameugua “Alisema.



Akizungumzia changamoto ambazo wamekuwa wakikumbana nazo,Meneja huyo
alisema ni uelewa mdogo wa wananchi hasa maeneo ya vijijini na
katakuchangamkia fursa za mfuko huo.


Habari kwa Hisani ya Blog ya
Kijamii ya Tanga Raha