Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

May 12, 2017

Guterres: Mazingira yameimarika Somalia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ameambia kikao cha kimataifa kinachojadiliana hatma ya Somalia kuwa mazingira nchini Somalia hivi sasa yameimarika na kwamba taifa hilo linaweza kufaulu katika yale linalotaka kufanya.

Amesema nchi hiyo kwa sasa ina serikali ambayo inaweza kuaminika na mipango yenye maana.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema Jumuia ya Kimataifa ina nafasi kubwa kuisaidia Somalia.
Hata hivyo Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed Farmajo ameonya kuwa mapambano dhidi ya wapiganaji wa Al Shabaab yanaweza kuendelea kwa miongo kadhaa iwapo vikwazo vya silaha havitaondolewa.
Mkutano huo wa siku moja ulizungumzia pia tatizo linaloikabili Somalia la athari za ukame ambazo zinageuka kuwa baa la njaa.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP