Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

May 6, 2017

Hali ya Mbunge wa CHADEMA Siyo Nzuri, Alazwa Muhimbili

Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche alifikishwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jana akitokea Dodoma kwa ajili ya matibabu baada ya kyzidiwa ghafla.

Mbunge huyo anasumbuliwa na  uvimbe ambapo mdogo wake, Edward Heche amesema kuwa kaka yake alianza kupatwa na maumivu makali juzi (Jumatano) akiwa Dodoma ndipo alipokwenda kwa ajili ya kumsaidia.
“Nilifika Dodoma saa tisa nikamkuta anatibiwa katika Hospitali ya Bunge hali yake haikuwa nzuri alikuwa analalamika kuwa maumivu yalizidi, tukampelekea Hospitali ya Mkoa bado aliendelea kulalama huko akapewa dawa za kupunguza maumivu lakini haikusaidia tulipoandikiwa kuja Muhimbili,” amesema na kuongeza;
“Hali ya Heche sio nzuri, tatizo ni kwamba alifanyiwa upasuaji kwenye uvimbe uliokuwa pajani lakini kwa bahati mbaya inaonekana baadhi ya nyuzi ziliachia na ndiyo inamsababishia maumivu makali.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP