DAR ES SALAAM: Imevuja! Baada ya hivi karibuni kuamua kupima Ukimwi kutokana na skendo iliyokuwa ikimtafuna kwamba ameathirika na vipimo kuonyesha yupo salama, habari mpya ni kwamba mwanadada Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ kwa sasa amewekwa kinyumba na mtoto wa kigogo (jina linahifadhiwa kwa sasa, Risasi Jumamosi lina ubuyu kamili.
Chanzo ambacho ni ndugu wa karibu na Aunty Lulu kilidai kuwakwa sasa mwanadada huyo amewekwa kinyumba na mtoto wa kigogo huko Bagamoyo mkoani Pwani.
“Aunty Lulu sasa hivi mambo yake ni mazuri sana maana amewekwa kinyumba na mtoto wa kigogo aliyewahi kuwa balozi wa Tanzania nchini Malaysia, wapo Bagamoyo kwenye ‘apartment’ za mtoto wa huyo kigogo wanakula zao bata,” kilidai chanzo.
Ili kuleta mzani wa habari hii, Risasi Jumamosi lilifika nyumbani kwao na Aunty Lulu maeneo ya Afrikana-Mbezi ambapo liliambiwa hayupo amesafiri hivyo likachukua hatua ya kumpigia simu na kusema yupo Bagamoyo.
Alipoulizwa kuhusiana na kuwekwa kinyumba na mtoto wa kigogo alikuwa na haya ya kusema; “Ni kweli niko Bagamoyo na mpenzi wangu ambaye siwezi kumtaja jina, mwenyewe hataki mambo ya magazeti kabisa, ila mipango yetu ikikaa sawa, mtamjua tu shemeji yenu.
|
0 Comments