Mheshimiwa Balozi Asha-Rose Migiro (wanne kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Kamishna Mkuu wa TRA, Bwana Charles E. Kichere (watatu-kushoto). Kamishna Mkuu wa TRA na ujumbe wake wapo nchini Uingereza kwa safari ya kikazi, Ijumaa tarehe 5 Mei 2017 walipata nafasi ya kutembelea Ofisi za Ubalozi na kufanya mazungumzo na Mhemiwa Balozi. Wengine katika picha ni msaidizi wa Kamishna Bwana Masumbuko Mwaluko (watatu kulia), Bwana Said Kiondo(wpili kulia) Kaimu Mkuu kitengo cha  Utafiti cha Mamlaka ya mapato, Mkuu wa Utawala Ubalozini, Bibi Rose Kitandula, Mwambata wa Fedha Ubalozini Bwana Wema Kibona na Mwambata wa Uhamiaji Bwana Magnus Ulungi