KUELEKEA MFUNGO WA MWEZI MTUKUFU… Leila Rashid: Ni muda muafaka wa kumsitiri Mzee Yusuf!
 DAR ES SALAAM: Wakati tukielekea kwenye mwezi wa toba wa Mfungo wa Ramadhani, ni wazi kwamba wengi wetu, katika historia ya maisha yetu kuna sehemu tulipita njia ambazo siyo sahihi. Mimi na wewe tumeshawahi kufanya mambo ya kumchukiza Mungu, wakati mwingine tukijua kuwa tunatenda dhambi au bila kujua.


Ndiyo maana hakuna anayeweza kusimama na kusema kuwa, hajawahi kufanya dhambi, mtu huyo hayupo! Lakini salama yetu kwa Mungu ni pale tunapogundua kuwa tumetenda dhambi kasha tukaamua kutubu na kuahidi kutorudia madhambi yaleyale!
Kwa mfano, yawezekana wewe ulishawahi kuzini na kosa hilo linakuumiza moyoni kiasi kwamba unataka kurudi kwa mola wako akusamehe.
Ukifanya toba ya dhati, Mungu hana la kukufanyia zaidi ya kukusamehe. Na hicho ndicho tunachotakiwa kufanya!
Kwa maelezo hayo sasa, nataka kurudi kwenye lile ambalo nimedhamiria kuliandika hapa kuhusu mwimbaji mahiri wa Muziki wa Taarab kupitia Kundi la Jahazi, Leila Rashid hasa kuelekea mwezi wa toba.
Wengi, hasa wale wadau wa muziki huo watakuwa wanamjua vizuri, anajua kuimba kiasi cha kuzikonga nyoyo za mashabiki wake.
Leila ni mke wa ndoa wa Mzee Yusuf. Lakini ikumbukwe pia Mzee Yusuf ana wake wawili, mwingine akijulikana kwa jina la Chiku.
Mzee Yusuf na Mkewe, Reila Rashid.
Huyu Chiku nikiri tu kwamba simfahamu kiundani maana yeye si mtu wa ‘media’ kama ilivyo kwa Leila. Kwa wanaowafuatilia wanandoa hawa, itakumbukwa kuwa miezi kadhaa nyuma, Mzee Yusuf aliyekuwa Mfalme wa Taarab Bongo na Mkurugenzi wa Bendi ya na kumgeukia Mungu.
Mzee Yusuf alikiri kwamba, kazi ya jukwaani aliyokuwa akiifanya ilikuwa kinyume na taratibu za Dini ya Kiislam hivyo akaona ni heri akaifuata njia iliyonyooka mapema kabla umauti haujamfi kia. Hilo ni jambo jema kabisa!
Wakati Mzee Yusuf akifanya hivyo, Leila naye alikuwa akifanya kazi hiyohiyo kwenye kundi Jahazi aliamua kuachana na mambo ya muziki hilohilo alilokuwa akiliongoza mumewe huyo.
Baada ya hayo kutokea, kumekuwa na maneno mengi mtaani hasa kwa wale waliofurahishwa na kitendo cha Mzee Yusuf kuacha muziki na kugeukia kazi ya kuitangaza Dini ya Kiislam.
Kilichokuwa kikisemwa ni kwamba, kama Mzee Yusuf ameamua kuacha muziki na kugeukia kazi za kidini, uhalali wa yeye kumuachia mkewe aifanye kazi ambayo kwa imani yake siyo sawa uko wapi?
Maneno hayo yaligonga akilini mwa Mzee Yusuf na hata alipozungumza na gazeti hili aliweka wazi kuwa, anafanya jitihada za kumrudisha mkewe kwenye njia iliyonyooka, akiamini kuwa haiwezi kuwa haraka kivile ila kuna siku watakuwa kundi moja.
Lakini sasa, cha kushangaza ni maneno anayoyatoa Leila, kwamba hata Mzee Yusuf ilimchukua muda mrefu kuacha muziki hivyo na yeye ipo siku ataacha! Maneno haya si ya busara kivile kutamkwa na mke wa mtu kama Leila.
Leila anajua wazi kuwa, mumewe kwa sasa anafanya kazi ya kidini, kuwataka watu kutenda yaliyo mema na kuacha maovu!
Sasa, katika mazingira hayo watu watamuelewaje wakati mkewe ambaye kidini yuko chini yake hayuko kwenye mstari ulionyooka?
Hivi mume polisi ambaye kila siku anatoka nyumbani na kwenda kudili na majambazi ataelewekaje kwenye jamii endapo na mkewe usiku anatoka na kwenda kushiriki matukio ya kihalifu na watu wanajua?
Haiwezi kuleta picha nzuri! Hicho ndicho kinachotokea kwa Mzee Yusuf, kazi yake anayoifanya inatiwa doa na mke wake hivyo umefi ka wakati wa Leila kumsitiri mumewe! Afanye uamuzi sahihi kwa wakati sahihi hasa kipindi hiki cha kuelekea mwezi mtukufu.
Akichelewa kuchukua uamuzi sahihi leo na Mungu akamchukua kesho, atajiweka kwenye mazingira magumu lakini pia atakuwa amemuweka mumewe kwenye wakati mgumu siku ya mwisho.
Nimefi kia hatua ya kuandika kwa sababu hivi karibuni niliona ‘clip’ mtandaoni ikimuonesha Mzee Yusuf akiwalingania watu, nikasema mashaallah!
Lakini ikanijia picha ya Leila na hapo ndipo nikajiwa na wazo la kumpa neno mwanamama huyu! Mimi nimenena, uamuzi anao Leila lakini pia Mzee Yusuf ajue kwamba siku ya mwisho atawajibika, ataulizwa alifanya nini katika kuwanyoosha wake na watoto wake? Nawatakia mfungo mwema Waislam wote!
Makala: Amran Kaima

Tazama Full Shoo ya Nay wa Mitego ‘Wapo Concert’ Dar Live – Mbagala