Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

May 16, 2017

Macron ataka marekebisho makubwa Ulaya

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametaka kufanyika marekebisho makubwa ndani ya bara la Ulaya kufuatia maongezi kati yake na Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel mjini Berlin.

Katika ziara yake ya kwanza kama Rais, Macron amesema wamekubaliana kwa pamoja kufanya kazi ndani ya Umoja wa Ulaya kwa ukaribu zaidi.
Kwa upande wake Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel amesema kutakua na hatua katika kuweka mambo sawa hususan masuala ya kodi.
Kabla ya kuelekea Ujerumani, Macron amemteua Edouard Philippe kuwa waziri mkuu mpya akitokea chama cha mrengo wa kati cha Republican.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP